Kuhusu Sisi
Tunajenga leo kwa ajili ya kesho iliyo bora. Fahamu zaidi kuhusu kampuni inayoleta mapinduzi kwenye sekta ya ujenzi na milki nchini Tanzania.
Kampuni Inayoaminika Kwa Ujenzi na Usimamizi Wa Majengo
Shayo Buildtech and Properties Ltd ni kampuni inayoongoza nchini Tanzania, inayotoa huduma kamilifu za ujenzi, usanifu wa majengo (architecture), na usimamizi wa milki (real estate). Tumejipanga kurahisisha mchakato wako wa ujenzi kuanzia wazo hadi kukamilika.
Lengo letu ni kutoa huduma bora zinazozingatia wakati, bajeti ya mteja, na viwango vya kimataifa huku tukitumia wataalamu wenye uzoefu na vifaa bora vya kisasa.
Dira Yetu (Vision)
Kuwa kampuni inayoaminika na kuongoza zaidi katika utoaji wa suluhisho la uhakika kwenye sekta ya ujenzi na milki Afrika Mashariki, kwa ubunifu na viwango vya juu.
Dhima Yetu (Mission)
Kutoa huduma bora na za kisasa za ujenzi, usimamizi wa mali na usanifu majengo kwa kuzingatia weledi, gharama nafuu, na ubora usio na shaka.
Maadili (Core Values)
Tunaamini katika Uaminifu (Integrity), Ubora wa Kazi (Quality Workmanship), Uwazi kwa Mteja (Transparency), na Uwasilishaji kwa Wakati (Timely Delivery).
Kwa Nini Utuchague?
Tunatoa huduma zinazolenga matokeo chanya, kwa kuhakikisha kila mradi unakidhi matarajio na viwango vyako.
-
Wataalamu Wabobezi
Tuna timu ya wahandisi, wasanifu majengo, na mameneja miradi walio na uzoefu wa kutosha.
-
Ubora Usio na Shaka
Tunatumia vifaa halisi (standard materials) na teknolojia za kisasa ili kutoa majengo imara yanayodumu muda mrefu.
-
Kukabidhi Miradi Kwa Wakati
Tunaheshimu muda wako. Tunahakikisha kila mradi unamalizika ndani ya mkataba na makubaliano yetu.
Upo Tayari Kuanza Mradi Wako?
Wasiliana na timu yetu ya wataalamu leo upate ushauri wa bure pamoja na makadirio ya gharama (Quotation) ya mradi wako.
Wasiliana Nasi

